Lady Jaydee Aitilia Shaka Amani Ya Tanzania

Msanii mkongwe wa muziki wa bongo fleva Lady Jaydee amefunguka na kusema kwa hali ilivyo sasa Tanzania ni wazi kuwa amani haipo kama alivyokuwa kipindi cha nyuma na kudai hali hiyo inaleta hofu miongoni mwa wananchi.
Lady Jaydee alisema hayo kwenye kipindi cha Planet bongo na kusema kitendo cha Mbunge Tundu Lissu pamoja na Meja Jenerali mstaafu wa JWTZ, Vincent Mritaba kupigwa risasi na watu wasiojulikana ni wazi kuwa amani ya nchi haipo.
"Ni kweli Tanzania hakuna amani kwa sababu kitendo cha mtu kupigwa risasi hadharani inatishia amani ukizingatia kuna wasanii wengine walikuwa wanatekwa unaogopa, sehemu yenye amani vitu kama hivyo haviwezi kutokea, na kitendo cha Meja mstaafu wa JWTZ kupigwa naye risasi inaongeza kabisaa Tanzani kuwa amani haipo naweza kuwa sina la kusema ila nikaishia kusikitika tu" alisema Lady Jaydee
Aidha Lady Jaydee anasema matukio haya yanaotoa picha mbaya kuwa kama nchi tunakokwenda si sehemu nzuri
Mbali na hilo Lady Jaydee kwa sasa ameachia video ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la 'I miss you' uliotengenezwa na mtayarishaji Man Water kutoka Combination Soound.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment