
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemwachia huru Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na wenzake watatu waliokuwa wanakabiliwa na shtaka la kushindwa kutunza silaha.
Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha, amesema mahakama imechukua uamuzi huo baada ya kupitia maelezo ya ushahidi uliotolewa na Pande zote mbili na kubaini kuwa upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha pasipo shaka.
“Nimeamua kumuachia huru Gwajima na wenzake watatu katika kesi yao ya kushindwa kutunza silaha kwani ushahidi haukufikia kiwango
kinachotakiwa kwani upande wa Jamhuri haujaweza kuthibitisha maelezo ya ushahidi wao,” amesema Hakimu Mkeha.
Askofu Gwajima alikuwa anakabiliwa na shtaka la kutohifadhi vizuri silaha huku wenzake George Mzava, Msaidizi wa Askofu Gwajima, Yekonia Bihagaze (39) na Georgey Mzava wao walikuwa wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa wakimiliki bastola aina ya berretta pamoja na risasi 20 kinyume cha sheria


0 comments :
Post a Comment