Mwenyekiti wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku amesema kuwa ana imani mchakato wa Katiba Mpya utaendelea huku akionya kasoro zilizojitokeza wakati wa mchakato huo zifanyiwe kazi ili kupata katiba itakayoridhiwa na wananchi wengi.
Suala hilo la upatikanaji wa Katiba Mpya pia limezungumzwa na baadhi ya wanazuoni wakiwa na mitazamo tofauti kuhusu umuhimu wake.
Katiba Mpya inazungumziwa na makundi mbalimbali ya kijamii nchini kuhusu umuhimu huo atika kuendesha shughuli za nchi kwa misingi ya kisheria hususan kwa kuzingatia kuwa Katiba ya nchi ndiyo sheria mama.
Mwenyekiti wa taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku ameweka bayana kuhusu masuala
yanayohitaji kuangaliwa upya katika upatikanaji wa katiba mpya ambapo amesema, inatakiwa kuwa ile yenye kukubaliwa na wengi badala ya kupelekwa bungeni na kupigiwa kura za Hapana na Ndiyo.
Amesema, anaamini wakati muafaka utakapofika, rais Magufuli ataliangalia suala la Katiba kwa umuhimu wake, na kuipeleka kwa wananchi kama itampendeza kwaajili ya kupigiwa kura huku akisisitiza kuwa mapungufu yaliyopo ni lazima yafanyiwe kazi.
Kusitishwa kwa mchakato wa kupata Katiba mpya ya Tanzania kumeendelea kuzua mijadala yenye mitazamo tofauti .
0 comments :
Post a Comment