Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewajia juu IGP, Simon Nyakoro Sirro pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba na kusema kama wao pia hawawajui watu wasiojulikana na wahalifu hao basi hawapaswa kuwepo ofisini.
Lema amesema hayo leo akiwa jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari na kusema kuwa haya mambo ambayo yanaendelea nchini sasa ikiwepo watu kuuwawa, viongozi kufuatiliwa na watu wasiojulikana na kutishiwa maisha yao yana mwisho na kusema familia, wananchi wapenda haki na wanachama hawawezi kuona maisha ya ndugu zao yakiwa mashakani wakaendelea kukaa kimya.
“Ukiangalia kauli za Waziri Mwigulu na sijui anafanya nini ofisini mpaka sasa, watu wanapotea, watu wanakufa maiti zinaokotwa , ndugu zangu matukio ya kutishiwa yamekuwa mengi leo tunaishi kwa mashaka hata ndugu wanatukimbia, unakwenda kuomba kulala kwa ndugu yako watu wanaogopa haya mambo yanatia uchungu, kama Rais hajui watu wanaotenda mambo haya anamwachaje Sirro kazini” alisema Lema
0 comments :
Post a Comment