Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema) amewasilisha ushahidi mwingine kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu tuhuma za ununuzi wa madiwani wa Chama hicho.
Madiwani hao nane wa Chadema wamejiuzulu kwa kile walichoeleza kumuunga mkono Rais John Magufuli jambo ambalo Nassari anadai siyo kweli bali walinunuliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo nje ya ofisi ya Takukuru Upanga jiji ni humo amesema, ” huu ni ushahidi wa tatu na kadri upepelezi ukiwa unaendelea nitaleta mwingine, hii ni kama filamu ya Isidingo.”
Nassari amesema alitarajia Rais John Magufuli angewachukulia hatua wateule wake wanaohusishwa katika sakata hilo ili kupisha uchunguzi uweze kufanyika kwa uhuru.
“Tunajiuliza kwa nini Rais hawachukulii hatua DED, DAS au DC wote wa Arumeru kwa kutuhumiwa, watupeleke mahakamani na tungeomba suala hili lichukuliwe kwa uzito wake,” amesema Nassari
Naye Mbunge wa Ubungo, Saed Kubunea aliyeongozana na