Rais Magufuli leo. Alhamisi Oktoba 26, 2017 amefanya uteuzi wa wakuu wa mikoa sita nchini kufuata baadhi ya wakuu wa mikoa kustaafu kwa mujibu wa sheria.
Mbali na kuwateua wakuu hao wa mikoa, rais Magufuli pia amemteua mabalozi wawili akiwemo aliyekuwa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Ernest Mangu.
Katika nafasi za wakuu wa mikoa rais Magufuli amemkumbuka aliyekuwa waziri katika Wizara ya Fedha awamu ya nne, Adam Malima anayekwenda kuwa mkuu wa Mkoa wa Mara pamoja na aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti ambaye sasa anakwenda kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara.
Wengine ni pamoja na Joakim Wangabo anayekwenda kuwa mkuu wa mkoa wa Rukwa, wakati katika Mkoa wa Geita, Robert Gabriel anachukua mikoba hiyo huku Cristin Mdeme akipokea mikoba ya Jordan Rugimbana na Gelasius Byakanwa alienda kuwa mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
Utawala
0 comments :
Post a Comment