Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limeeleza kushtushwa kwake na hatua ya Tanzania kuanguka kwa nafasi 11 katika viwango vya soka duniani vilivyotolewa jana na FIFA kutoka nafasi ya 125 hadi nafasi ya 136.
Kaimu katibu mkuu wa shirikisho hilo, Wilfred Kidao amesema wao kama shirikisho hawakugemea kama Tanzania ingeshuka kwa kiwango hicho huku akiweka wazi kuwa hivyo ni viwango ambavyo vinawaumiza siyo wao tu bali wadau wote wa soka nchini.
Kidao amesema shirikisho hilo limeweka mikakati ya kuhakikisha Tanzania inapanda katika viwango hivyo kwa kutafuta mechi nyingi za kirafiki za ugenini pamoja na kutafuta timu ambazo ziko kwenye nafasi bora