Mbunge Wa Mikumi Aangua Kilio

 

Kufuatia kuuwawa kwa kijana Saidi Salim Mheka, mwenye umri wa miaka 17, Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ameshindwa kujizuia na kuangua kilio hadharani kwenye mkutano aliokuwa amefanya na wananchi wa kijiji cha Ruhembe wilayani Kilosa Mkoani Morogoro.

Kufuatia tukio hilo, Mhe. Haule amemewaomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Waziri Mkuu kuchukua hatua kabla ya wananchi hawajajichukulia hatua wenyewe.

Kijana huyo aliyemaliza kidato cha nne katika shule ya Sekondari Ruhembe, ameuwawa kwa kupigwa risasi na polisi wa Kanda Maalum ya Morogoro kwa kutuhumiwa kuhusika na mauaji ya kibiti.

Baba wa mtoto huyo, ndg Saidi Mheka akishirikiana na wananchi wamegoma kuzika mwili wa kijana huyo akidai na polisi wa kitengo maalumu kwa madai kuwa alikuwa ni mhalifu wa Kibiti.

Aidha Kamanda wa Polisi Kanda ya Morogoro, Urlich Matei amesema kuwa, kijana huyo alikuwa anajihusisha na ugaidi na wanaendelea kufuatilia undani wa tukio hilo maana kuna vijana wengine wanaodaiwa kujihusisha na vitendo hivyo vya kiharifu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment