MFANYABIASHARA MAARUFU-MZALENDO WA IRINGA ADAIWA MILIONI 296, APANDISHWA KIZIMBANI


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Iringa leo imempa dhamana mfanyabishara wa mjini Iringa Rodrick Allon maarufu kwa jina la Mzalendo na wasaidizi wake wawili wanaodaiwa kutumia vibaya mashine za kielektoniki za kodi (EFD) na kushindwa kurejesha kodi ya zaidi ya Sh Milioni 296 serikalini.

Mzalendo na wasaidizi wake hao,  Exaud John na Oswald Njole hawakutokea mahabusu (walikuwa nje bila masharti yoyote) wakati kesi yao ikitajwa kwa mara ya kwanza mahakamani hapo juzi na shauri la dhamana lilipokuwa likisikilizwa jana.

Mbele ya Hakamu Mkazi wa mahakama hiyo, Richard Kasele, wakili wa washitakiwa hao, Moses Ambindwile aliiomba mahakama hiyo iwape dhamana wateja wake hao kwa masharti yanayotekelezeka kwa mujibu wa sheria.

“Naomba mahakama iwaruhusu kudhaminiwa na  wadhamini ambao ni wakazi wa mjini Iringa watakaoweka bondi ambayo ni nusu ya thamani ya kiasi wanachodaiwa kutokirejesha serikalini ambacho ni Sh 296,985,950.82,” alisema.

Wakili wa upande wa mashtaka anayeiwakilisha Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Cherubin Ludovick hakuwa na pingamizi la maombi hayo ya dhamana.

“Suala la dhamana itolewe kwa masharti gani, ni uamuzi wa mahakama, naomba mahakama ijielekeza na maombi yaliyoletwa na upande wa uetetezi lakini ihakikishe haki inatendeka kwa pande zote mbaili wakati ikifanya uamuzi,” alisema.

Akitoa uamuzi wa dhamana hiyo, Hakimu Mkazi Kasele alisema kwa kuwa hakuna upande unaopinga washitakiwa hao wanaodaiwa kufanya makosa hayo kati ya mwaka 2015 na 2016 kupewa dhamana, mahakama hiyo inawapa dhamana kwa masharti mawili.

Alitaja masharti hayo kuwa ni kila mshatakiwa awe na wadhamini wawili wakazi wa Iringa watakaoweka bondi ya Sh Milioni 50 au Sh Milioni 50 taslimu kwa kila mshatakiwa.

Alisema kesi hiyo namba 23 ya mwaka 2017 itatajwa tena mahakamani hapo Desemba 12, mwaka huu.

Mzalendo ni mfanyabishara maaarufu mjini Iringa wa vifaa vya ujenzi, nyumba za kulala wageni, usafirishaji na ni msambazaji wa vinywaji vya aina mbalimbali
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment