MEYA MANISPAA YA IRINGA AACHIWA KWA DHAMANA, WANA CHADEMA WENGINE WATANO WANYIMWA DHAMANA



MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Iringa, Alex Kimbe (Chadema) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya wilaya ya Iringa mapema leo akituhumiwa kutishia kumua kwa bastola, Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Manispaa ya Iringa, Alphonce Muyinga.

Pamoja na Kimbe, Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imewasomea mashtaka matatu wafuasi wengine watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) waliyofanya Novemba 19 wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Kitwiru, Iringa mjini.

Wakati meya huyo ameachiwa kwa dhamana na mahakama ya wilaya Iringa baada ya kusota rumande kwa siku tatu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imewanyima dhamana wafuasi hao watano kwa kuwa kati ya makosa matatu wanayotuhumiwa kuyafanya kosa moja halidhaminiki.

Mwendesha Mashtaka  wa Polisi, Aristeck Mwinyikheri alisema Kimbe aliyefikishwa mahakamani hapo kwa kesi namba 189 ya mwaka 2017 anashitakiwa kutishia kumuua kwa Bastola Katibu huyo wa UVCCM kwa katika tukio lililotokea Novemba 26 mwaka huu katika kata ya Kitwiru, mjini Iringa wakati shughuli ya uchaguzi mdogo wa udiwani wa kata hiyo ikiendelea.

Mwinyikheri alisema meya huyo  alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 89 (2) (a) cha kanuni za adhabu.

Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Iringa John Mpitanjia alisema shauri hilo litarudi tena mahakamani hapo Desemba 12, mwaka huu wakati Meya huyo aliyedhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa akikana kutenda kosa hilo.

Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa, wafuasi hao watano wa Chadema walioshitakiwa kupitia kesi namba 190 ya mwaka 2017 na kunyimwa dhamana ni pamoja na Martha Robert, Leonard Kulijira, Esau Bwire, Christopher Jevas na Samwel Nyanda.

Mbele ya hakimu mkazi wa mahakama hiyo,  Richard Kasele , mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo Chakila Felix alisema washitakiwa hao wanatuhumiwa kujeruhi, kuteka na kufanya unyang’anyi kwa kutumia nguvu.

Felix alisema watuhumiwa hao wanatuhumiwa kumjeruhi Dick Frank na kumnyang’anya simu yake ya mkononi.

Mahakama hiyo imewarudisha rumande kwa kuwa kosa la unyang’anyi kwa kutumia nguvu halina dhamana na shauri lao litarudi tena mahakamani hapo Desemba 12, mwaka huu
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment