Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro, imewanyima dhamana wabunge wa CHADEMA Peter Lijualikali, Suzan Kiwanga na wengine 34, na kuwarudisha mahabusu hadi Desemba
Walifikishwa kituoni hapo Jumanne Novemba 28,2017 baada ya kukamatwa Jumapili Novemba 26,2017 saa tano usiku wakituhumiwa kufanya fujo zilizohusisha uharibifu wa mali za umma.
Vurugu hizo zilitokea baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Sofi wakituhumiwa kuchoma moto ofisi za taasisi za umma yakiwemo majengo ya shule ya msingi Sofi, ofisi ya mtendaji kata na nyumba ya walimu wa shule hiyo.
Lijualikali ambaye polisi ilisema naye anahusishwa na vurugu hizo, amejisalimisha polisi leo Alhamisi Novemba 30,2017 saa nne asubuhi.
0 comments :
Post a Comment