ANC Yapata Mwenyekiti Mpya Kumrithi Zuma

Chama cha African National Congress (ANC), Afrika Kusini kimemchagua Cyril Ramaphosa, kuwa mwenyekiti mpya wa chama hicho akimrithi Jacob Zuma.
Ramaphosa amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama tawala nchini Afrika Kusini ANC leo baada ya kufanyika uchaguzi.
Makamu huyo wa  rais aliyeibuka mshindi alikuwa na upinzani mkali na waziri wa zamani Nkosazana Dlamini-Zuma, mke wa zamani wa  Zuma.
Kulikuwa na  mvutano, hisia zikipanda, wajumbe wakipiga kelele kupinga taratibu za upigaji wa kura.
Uwaniaji madaraka umeleta mvutano  wa kisiasa nchini humo  hali inayoleta hofu kuwa ANC inaweza kugawanyika kabla ya uchaguzi wa 2019.
Ramaphosa ameibuka mshindi kwa kupata kura  2,440 huku mpinzani wake  Dlamini-Zuma akipata kura 2,261.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment