
Kamanda wa polisi mkoa wa Dar, Lazaro Mambosasa amesema hakuna ushahidi kuwa waliowapiga wananchi Ukonga ni askari, na ametaka mtu yeyote mwenye ushahidi aupeleke.
Ameelezea watuhumiwa hao walipokuwa wanawapiga wananchi walikuwa wamevaa 'mask' na hakuna askari polisi anayeweza kuvaa hivyo
"Hakuna ushahidi wowote, hakuna askari wa polisi anayeweza kwenda kumpiga mtu huku akiwa amevaa mask." Amesema Mambosasa
Mnamo Oktoba 22 mwaka huu watu wanaodaiwa kuwa ni askari wa kutuliza ghasia walivamia na kuwapiga wananchi wa eneo la Ukonga Mombasa mara baada ya askari mmoja kuuawa
0 comments :
Post a Comment