Mamilioni Yakamatwa Airport Yakiingizwa Nchini Kinyume Na Sheria

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema zaidi ya dola bilioni moja zimeshikwa zikiingizwa nchini kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.
Akiwa jukwaani mjini Dodoma leo wakati akizindua tawi la Benki ya CRDB, Rais Magufuli ameweka wazi kuwa amepata taarifa zaidi ya kiasi cha dola bilioni moja zimeshikwa zikiingizwa nchini kinyume na sheria kupitia uwanja wa ndege wa Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es salaam.
“Ninapozungumza tu sasa hivi nimepata taarifa zaidi ya bilioni moja dola zimeshikwa Airport zilikuwa zinaingizwa Tanzania kwasababu Tanzania kimeshaonekana ni kichaka cha fedha za kigeni” amesema Rais Magufuli.
Kwa upande mwingine Rais amezitaka mahakama za biashara nchini kuharakisha kesi zinazohusiana na kesi za mikopo ili kuwezesha Benki kuendelea kutoa mikopo. Pia ameongeza kuwa baadhi ya wakopaji hutumia fedha hizo hizo za mikopo kuchelewesha kesi, hivyo mahakama zinatakiwa kutoa hukumu kwa wakati.
“Nawahimiza wananchi kulipa madeni yao kwa wakati, dawa ya deni kulipa, na niziombe Mahakama za biashara kuharakisha kesi zinazohusu mikopo, mtu anapopelekwa amekopa na anatakiwa kuuziwa jengo lake au kufirisiwa, unachelewesha nini toa amri watu wakauze ilikusudi Benki ziendelee kukopesha wengine”amesema Magufuli.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment