December 3 2017 club ya Simba iliingia katika historia mpya na kutangaza kubadili mfumo wa uendeshaji wa club hiyo kutoka mfumo wa sasa na kuipeleka club katika mabadiliko ya kiuendeshaji kwa mfumo wa hisa sambamba na kumtangaza mshindi wa zabuni ya uwekezaji ndani ya Simba SC.
Simba imemtangaza mfanyabiashara Mohamed Dewji ambaye anatajwa katika list ya mabilionea wa Afrika kuwa ndio mshindi wa zabuni ya uwekezaji wa timu hiyo kwa dau la Tsh bilioni 20, kwa mujibu wa kanuni zilizotangazwa na Waziri mweye dhamana ya michezo MO Dewji ataruhusiwa kumiliki asilimia 49 ya hisa za Simba na wanachama asilimia 51.
Afisa habari wa Simba Haji Manara baada ya club yao kupiga hatua hiyo amepost ujumbe flani hivi wa kuwatania watani zao wa jadi Yanga ambao bado wanategemea michango ya wanachama, post ya manara ipo hivi kapost picha ya mabilionea mbalimbali wanaomiliki vilabu.
0 comments :
Post a Comment