Manchester United Yapigwa Fitina

Mashabiki wa Manchester United wamelipuka mtandaoni kwa hasira wakilalamika kuhusu gharama za tiketi ya kuingia uwanjani kuangalia mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Sevilla na Timu yao.

United wanatarajia kusafiri kuelekea Hispania katika mchezo wa kwanza wa 16 bora ambapo inadaiwa kwamba Sevilla wametangaza kiingilio cha £133 kwa mashabiki wa ugenini watakaokwenda siku hiyo.

Mashabiki wengi wa United wanaonekana kukerwa sana na kiasi hicho cha pesa wengine wakidai kwamba gharama za safari wanazotumia kutoka Uingereza kwenda Hispania ni ndogo kuliko pesa ya tiketi.

Uwanja wa Ramon Sanchez Pzijuain ndio utakaopigwa mtanange huo na habari zinasema siti kwa ajili ya wageni zipo 2650 tu na hao watakaofika hapo itawapasa kutoa kiasi hicho cha pesa kuingia uwanjani.

Mashabiki wa Manchester United tayari wameomba uongozi wa Manchester United Supporters Trust (MUST) kuwasaidia kuhusu tiketi la pambano hilo lla sivyo wengi hawatasafiri kuelekea Hispania.

Sevilla watakuwa wenyeji wa Manchester United usiku wa tarehe 21 February katika mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora kabla ya timu hizo kurudiana wiki mbili baadae.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment