Ramsey Atembelea Kaburi La Marehemu Kanumba

Muigizaji kutoka nchini, Nigeria Ramsey Nouh ambaye alifanya movie moja itwayo ‘King Of Devil’ na marehemu Steven Kanumba, ametua nchini Tanzania wiki hii kwaajili ya kukutana na wasanii wa Bongo Movies ambapo jana alipata nafasi na kunywa chai na Mama Kanumba na baadaye kwenda makaburini kwaajili na ibada.
Wakiwa makaburini hapo, Ramsey na Mama Kanumba walitumia muda mwingi kukumbatiana na kulia kwa huzuni jambo lililoteka na kuvuta hisia za watu wengi. 
Mbali na tukio hilo, Ramsey alizidisha machungu kwa mama huyo baada ya kuanza kutamka maneno kama anazungumza na marehemu Kanumba ambapo alimueleza mambo yenye kuumiza.
“Steven, kwa mara ya mwisho tulizungumza sote tukiwa hai lakini leo nimesimama kando yako ukiwa umelala chini ya mchanga hujitambui, kwangu ni zaidi ya msiba na kwa kweli nimeshindwa kuhimili jambo hili, najua huko uliko unaumia sana hususan ukizingatia ukweli kwamba tasnia ya filamu za Kitanzania inakufa,” alisema Ramsey katika mazungumzo yale na Kanumba aliyoyatoa kwa hisia kali hali iliyomsababishia Mama Kanumba maumivu makali. 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment