Takukuru Kuwafatilia Wabunge Wanaojizulu Ubunge



TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imesema inafuatilia tuhuma za rushwa zinazotajwa dhidi ya wabunge wanaohama vyama vyao.

Msingi wa kauli hiyo ya Takukuru ni swali lililoulizwa na gazeti hili kwa msemaji wa taasisi hiyo, Mussa Misalaba kutokana na kuwapo kwa tuhuma hizo, hasa kutoka upande wa upinzani, kwamba kuondoka kwa wabunge na wanasiasa wao ni mkakati unaoratibiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), ukiwa umeambatana na ama rushwa ya fedha au ahadi za vyeo.


Katika hilo, Misalaba alikiri kusikia na hata kuziona tuhuma hizo kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii na kusisitiza kuwa wao kama Takukuru wako macho na wanafuatilia mahala popote penye harufu ya rushwa.


Ingawa Misalaba alikiri chombo chao kukabiliwa na changamoto ya kukamata watuhumiwa endapo jambo la rushwa limefanywa katika misingi ya ‘ugiza giza’, lakini alisisitiza endapo wataiona na hata kuwa na ushahidi, hawatasita kuwachukulia hatua wahusika.


Kauli hiyo ya Takukuru imekuja katika wakati ambao si tu wapinzani bali hata jamii imegubikwa na hisia kwamba wabunge na hata baadhi ya wanasiasa wanaohama kutoka upinzani msingi wake ni rushwa, huku nia kubwa ikiwa ni kudhoofisha upinzani ili ufike mwaka 2020 ukiwa dhaifu.


Kwa bahati mbaya, hisia hizo zimetawala zaidi baada ya wabunge wawili wa upinzani waliokuwa wakiunda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Godwin Mollel wa Siha (Chadema) aliyejiuzulu nafasi hiyo na kujiunga CCM na kabla ya hapo Mbunge wa Kinondoni, Dar- es Salaam, Maulid Mtulia (CUF).


Mwanzilishi wa hamahama hiyo, Lazaro Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM), alipotangaza kujiunga Chadema, hisia zilikuwa ni tofauti na hizo.


Wafuatiliaji wa mambo wanasema kilichochochea zaidi kuwapo kwa hisia za namna hiyo, ni maandiko ya watu kama Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob na wengine, kwamba CCM imeandaa mkakati mzito wa kuchukua wabunge wa upinzani takribani 20 na hata kudai yupo kiongozi mmoja ambaye amekuwa akipiga simu kuwashawishi baadhi yao na kwamba wamemrekodi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment