Takukuru Yamuachia Aliyekuwa Rais Wa CWT

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini imemuachia aliyekuwa Rais wa Chama cha walimu (CWT) Gratius Mukoba bila kumfikisha mahakamani. 
Kamanda wa Takukuru mkoa wa Dodoma Emma Kuhanga  amesema Mukoba hakupelekwa mahakamani kama ilivyotakiwa.
 
"Hapana hatujampeleka mahakamani, tulishamuachia,....ni hivyo kwamba mahakamani hakupelekwa," amesema Kuhanga
 
Mwishoni mwa wiki Takukuru ilimkamata Mukoba kwa madai ya kujihusisha na ugawaji wa rushwa kwa wajumbe na alitarajia kufikishwa mahakamani leo.
 
Alipoulizwa iwapo Rais huyo wa zamani wa CWT ataitwa tena ama taasisi yake imeona hana hatia, Kamanda Kuhangwa amesema "wewe elewa kuwa hatujampeleka mahakamani lakini tumemwachia,"
 
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment