Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Tanzania inautaka Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi wa kina, ulio wazi na wa ukweli juu ya vifo vya Wanajeshi 14 wa Jeshi la Wananchi waliouawa huko Jamhuri ya Congo December 8, 2017.
Amesema hayo leo December 14, 2017 wakati akiongoza mamia ya wanajeshi, viongozi wa serikali, na familia za Mashujaa hao na kueleza kuwa serikali inatumaini Umoja wa Mataifa utafanya hivyo haraka ili haki iweze kutendeka.
Ametoa pole kwa Jeshi, familia za wafiwa na Watanzania kwa ujumla na kuwaasa wanajeshi kuwa yaliyotokea DRC yasiwakatishe tamaa katika kutimiza wajibu wao huko Congo na kwingineko ambako wanatoa msaada huo.
0 comments :
Post a Comment