
Umaarufu wa rais wa Tanzania John Pombe Magufuli umeshuka kwa asilimia 25 kulingana na utafiti wa kura ya maoni iliofanywa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Kwa mujibu wa shirika la Twaweza lililofanya kura hiyo Watanzania 7 kati ya kumi wanaunga mkono utendakazi wa rais Magufuli ikiwa ni sawa na asilimia 71 ikilinganishwa na asilimia 96 mwaka 2016.
Hatahivyo ripoti hiyo ya Twaweza inaonyesha kuwa rais Magufuli bado ana umaarufu miongoni mwa watu wazima walio na umri wa miaka 52 kuendelea kwa asilimia 82 huku wale ambao hawana elimu ya kutosha wakimuunga mkono kwa asilimia 75 huku walio maskini wakimuunga kwa asilimia 75.
Miongoni mwa vijana walio chini ya umri wa miaka 30, ni asilimia 68 pekee waliomuunga mkono, asilimia 63 wakiwa wasomi na asilimi 66 wakiwa matajiri.
Kulingana na mkurugenzi mkuu wa Twaweza Aidan Eyakuze, kushuka kwa umaarufu wa rais huyo kunaonyesha kupungua kwa uaminifu wa wapiga kura kuhusu wanasiasa wao.
''Kushuka kwa viwango hivyo pamoja na vile vya umaarufu katika kura ya maoni miongoni mwa wanaiasa kunatoa ujumbe kwamba raia wanaendelea kupoteza imani yao na viongozi wa kisiasa''.
0 comments :
Post a Comment