Zijue Gharama Za Kumnunua Mbunge Ajiuzuru






Kumekuwa na hamahama ya wanasiasa kutoka chama kimoja kwenda kingine hasa wabunge na madiwani ambao walitumia nguvu na maarifa mengi kupata viti hivyo.

Kuna sababu wanazitoa ikiwemo kuunga mkono juhudi zinazofanywa na  chama wanachohamia.

Inasemekasna kwamba kuna baadhi ya wabunge wananunuliwa ili kujiuzulu nafazi ya ubunge na kuhamia chama kingine .

Hapa chini nimekuwekea mahesabu ya haraka haraka  ya fedha anazopoteza mbunge kwa kujiuzulu nafasi yake ya ubunge.

Mshahara Wa mbunge kwa mwezi ni Tsh milioni 11,Mpaka 2020 sawa na miezi 36 mbunge huyu atapoteza takribani mil 396.

Mbunge huyu itampasa alipe madeni yake yote kama vile mkopo wake wa "Bunge loan" wanaopewa na bank ya NMB wa zaidi ya mil 500 pamoja na riba haitapungua mil 600.

Mbunge huyu ataacha posho zaidi ya mil 120 kwa miezi 36 iliyobaki (Sitting allowance) ili
Mbunge huyu baada ya miaka 5 angelipwa pension ya Tsh 160,000,000 ataiacha ili kumuunga mkono Rais. 

Mbunge huyu atapaswa kurejesha mkopo wa Gari wa Tsh milioni 90.

Kwa maana hiyo mbunge aliyejiuzulu atapoteza zaidi ya Tsh Bilioni 1.366 (Bilioni moja na milioni mia tatu sitini na sita). 

Kwa hiyo kama ni kweli mbunge ananunuliwa atakuwa anapigiwa mahesabu ya kufidiwa Gharama hizo za Bilioni 1.366 na Nyongeza juu
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment