Akamatwa Kwa Tuhuma Za Kubaka Mbuzi

Mtu mmoja nchini Kenya mwenye umri wa miaka 35 amefikishwa mahakamani akituhumiwa kubaka mbuzi wawili wa jirani yake, na kisha kuwaua.
Tukio hilo limetokea Januari 13 mwaka huu, baada ya watu kumuona akiwaburuza mbuzi hao kutoka porini ambako anahisiwa kufanya tukio hilo, katika eneo la  Kangundo
Waendesha mashtaka wametaka mbuzi hao wapelekwe kufanyiwa vipimo ili kubaini kama kweli wamefanyiwa kitendo hicho, na kutaka mshtakiwa kupatiwa matibabu baada ya kulalamika alipigwa vibaya na polisi walipoenda kumkamata.
Kesi hiyo imehairishwa mpaka Januari 29, na mshtakiwa kupewa dhamana ya shilingi 100,000 za Kenya.
Sheria za Kenya zinamtaka mtu atakayekutwa na hatia ya kufanya ukatili kama huo kwa wanyama kwenda jela kwa miaka 14.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment