Dawasco Kulipa Fidia Nyumba Iliyoungua Buguruni

Mamlaka ya maji safi na maji taka jijini Dar es salaam DAWASCO imesema itamlipa fidia mmiliki wa nyumba iliyoungua moto jana maeneo ya Buguruni kutokana na moto uliosababishwa na shughuli za mamlaka hiyo.
Akiongea  kwenye eneo la tukio Mkurugenzi mtendaji wa DAWASCO Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema ofisi yake inaongea na mmiliki huyo ili kuona namna ya kumlipa kutokana na uharibifu uliotokea.
''Tunaongea naye kuona jinsi gani tutamlipa fidia kwa uharibifu huu uliotokea  ili aweze kuendelea na maisha yake na familia kama kawaida'', amesema Luhemeja.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Ilala Salum Hamduni amesema zoezi la kuziba bomba la gesi la Songasi ambalo liliungua juzi  usiku limefanikiwa na hali kwa sasa ni shwari baada ya kufanikiwa kuziba 'valve' zilizopasuka.
Tukio hilo la moto lilitokea juzi jioni katika eneo hilo la Buguruni Mnyamani baada ya mafundi wa DAWASCO kupasua kwa bahati mbaya bomba la gesi la Songasi ambalo lilisababisha kulipuka kwa moto huo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment