Mafuriko Yaleta Maafa Dodoma

Na Canal- Wazohuru
Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha Mwakisebe kata ya Kimaha wilayani chemba mkoani Dodoma amefariki dunia, huku watu wengine zaidi ya 2000 wakiwa hawana mahali pa kuishi baada ya nyumba zao kubomoka na nyingine kuzingirwa na maji, kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani humo.
Wilaya ya Chemba ni miongoni mwa wilaya mpya zinazopatikana makao makuu ya nchi Dodoma ambapo katika msimu wa mvua hizi za masika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Dodoma yamekuwa yakipata mvua nyingi zinazosababisha mafuriko na adhari mbalimbali kujitokeza ikiwemo kuharibika kwa miundombinu ya barabara.
Athari za mvua hizo zimejitokeza katika vijiji vya Olboloti,Kaloleni na Mrijo Chini ambavyo ndivyo vinavyodaiwa kuwa ndio vimeathiriwa zaidi na mafuriko hayo.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kijiji cha Olboloti  Abdalah Suti amesema kuwa mvua iliyonyesha katika maeneo yao ni kubwa na kwamba haijawahi kutokea tangu miaka ya 1960
Amiry Issa ni Mkuu wa zimamoto kituo cha Dodoma amesema kuwa kikosi kinaendelea na shughuli za uokozi kuzunguka vijiji hivyo huku akiwataka wananchi kutosogelea maeneo hatarishi
Akizungumzia hilo,Mkuu wa wilaya ya Chemba ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya hiyo, Simon Odunga amesema kuwa eneo wanaloishi wananchi hao ni eneo hatarishi kwani wanazungukwa na milima huku akiwataka wananchi waliojenga katika maeneo ya mabondeni kuhama mara moja.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment