Magufuli Aahidi Kutoa Bilioni 200 Kulipa Wanaoidai Serikali


Leo January 3, 2018 Rais Magufuli amesema kuanzia mwezi February mwaka huu madeni ya ndani ya nchi ya wanaoidai serikali yataanza kulipwa, na kwamba atatoa Tsh Bilioni 200 kufanikisha zoezi hilo na kuongeza kuwa hii itasaidia kuongeza uchumi.
Ameyasema hayo wakati amekutana na kuagana na Gavana wa Benki Kuu (BoT) anayemaliza muda wake Profesa Benno Ndulu aliyeongozana na Gavana mpya wa BoT Frolens Luoga Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo wote walipata nafasi ya kuzungumza.
“Nimepanga kuanzia mwezi ujao madeni yote ya ndani ya wanaoidai serikali yatakapokuwa yamehakikiwa, nitatoa Tshs Bilioni 200 ili yakalipwe. Ningeweza kutoa hata kesho au kesho kutwa ila ni lazima tuhakiki kwanza, uhakiki ukifanywa mapema, madeni yataanza kulipwa mapema, na kuwasaidia watu hawa kuendelea kufanya biashara zao.” – Rais Magufuli 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment