KIKOSI cha Majimaji leo Jumatano kinatarajia kuingia jijini Dar ikiwa ni muda mfupi kabla ya kuvaana na wapinzani wao Simba katika pambano la ligi ambalo litapigwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa.
Majimaji wanaodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Sokabet, inatua Dar ikiwa na kikosi kamili kwa ajili ya mchezo huo na Simba ambapo mchezo wao wa mwisho waliilazimisha sare Singida United ya kufungana bao 1-1.
Kocha msaidizi wa timu hiyo iliyo katika nafasi ya 12, Habibu Kondo ameliambia Championi Jumatano, kuwa wamekuja Dar kuhakikisha wanaendeleza mwendo wa kukusanya pointi kama walivyofanya kwenye michezo yao miwili ya mwisho dhidi ya Azam na Singida United kabla ya kuivaa Simba.
“Kesho (leo) Jumatano ndiyo tunatarajia kufika huko Dar kwa ajili ya kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya kucheza na wenyeji wetu Simba, tunawaheshimu wapinzani wetu kama timu kubwa lakini tunataka kufanya vizuri mbele yao.
“Tunajua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila tumejipanga vyema kwa ajili ya kupata pointi mbele ya wenzetu hao, tunakuja tukiwa kamili kwa maana ya kikosi chote na siku chache ambazo tutakaa huko zitatufanya kuzoea mazingira kabla ya kupambana na wapinzani wetu,” alisema Kondo.
0 comments :
Post a Comment