Mama Ajifungua Mtoto Mwenye Vichwa Viwili

HOSPITALI YA HALMASHAURI YA KAHAMA.
MKAZI wa wilayani Kahama mkoani Shinyanga, Lucia Juma (25), amejifungua mtoto wa ajabu mwenye vichwa viwili katika Hospitali ya Halmashauri ya Kahama.
Akiongea na Nipashe, Lucia alisema uchungu ulianza kumshika mchana na kwenda kituo hicho cha afya kwa ajili ya kujifungua, lakini ilipofika usiku hali ilikuwa mbaya na kupelekwa Hospitali ya Kahama kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
Alisema huo ni uzazi wake wa pili, uzazi wa kwanza alijifungulia nyumbani salama.Mume wa Lucia, Zuberi Dalali, alisema ameshangaa kuona mke wake amejifungua mtoto mwenye vichwa viwili na kwamba hilo ni jambo la ajabu kutokea katika maisha yake, lakini anamshukuru Mungu kwa kila jambo.
Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Fredrick Malunde, alikiri mwanamke huyo kufika katika hospitali hiyo akiwa na uchungu wa siku mbili na walimpatia dawa ya kuongeza nguvu ili aweze kujifungua salama, lakini ilishindikana.
Dk. Malunde alisema, aliposhindwa kujifungua kwa njia ya kawaida, walimsaidia kwa kuongeza njia na wakati mtoto anatoka alikuwa na vichwa viwili, akiwa salama. Aidha, Dk. Malunde alisema mtoto huyo alikaa siku moja na kufariki dunia kutokana na kushindwa kupumua vizuri.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment