Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo la Kinondoni ambaye pia mkurugenzi wa manispaa hiyo, Aron Kagurumjuli ameyatupilia mbali mapingamizi matatu yaliyowasilishwa na wagombea wa vyama vya Chadema, CCM na CUF.
Mapingamizi hayo ni kwa mgombea wa CUF, Rajab Juma kumwekea mgombea wa Chadema, Salumu Mwalimu, wakati Mwalimu yeye alimwekea Maulid Mtulia wa CCM na mgombea huyo wa chama tawala alimwekea mgombea wa SAU, Johnson Mwangosi.
Baada ya jana ofisi ya msimamizi wa uchaguzi kutoa barua ya utetezi kwa wagombea waliowekewa mapingamizi leo Jumanne imetoa majibu ya kuyatupilia mbali mapingamizi hayo.
“Tumeyatupilia mbali mapingamizi yao kwa sababu hayana mashiko, kilichobaki ni wagombea kwenda uwanjani wakapambane,” amesema msimamizi huyo.
0 comments :
Post a Comment