Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
MBOWE AHUDHURIA MAHAKAMANI KWENYE KESI YA SUGU & MASONGA
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe. Freeman A. Mbowe (MB) leo Jumatano tarehe 24 Januari 2018 amewasili Mbeya na muda huu ameingia Mahakama ya Mkoa wa Mbeya kwa ajili ya kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu CHADEMA Mhe. Joseph Mbilinyi na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga.
Mwenyekiti Mbowe ambaye ameongozana na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Mhe. Sophia H. Mwakagenda ameingia majira ya saa 3.30 asubuhi hii katika viunga vya Mahakama kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo na tayari ameingia kwenye chumba cha mahakama.
Habari CHADEMA
Kanda ya Nyasa
"Caytano Maytano"
Charles Francis M.
0 comments :
Post a Comment