Mbowe Aionya Tume Ya Uchaguzi




Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amefunguka na kuionya Tume ya Uchaguzi (NEC) kuhusu ukiukwaji, upuuziaji na uzalilishaji kwa wapinzania kwenye uchaguzi. 

Mbowe ametoa onyo hilo leo Januari 22, 2018 na kusema kuwa wao kama CHADEMA wameamua kurudi kwenye uchaguzi licha ya ukweli kwamba Tume ya Uchaguzi (NEC) mpaka sasa hawajakiri kwamba kulikuwa na makosa makubwa kwenye uchaguzi wa Kata 43 uliofanyika mwaka jana.

"Naionya Tume ya Uchaguzi (NEC) dhidi ya ukiukwaji, upuuzaji na uzalilishaji wa wapinzani kwenye uchaguzi. Ukiacha NEC, kimamntiki na kisheria wengine hawana mamlaka ya kusimamia uchaguzi kwa kuwa kuna chombo maalum chenye wajibu huo kisheria. Katika kata 26 mwaka jana tuliwaona wakuu wa mikoa na wilaya wakisimamia uchaguzi, wakielekeza maofia wa NEC, wakiamuru udhalilishaji wa wagombea, mawakala na hata viongozi wa vyama vya upinzani, jambo ambalo liliweka msingi mbaya wa kiusalama na kiutaratibu katika uchaguzi" alisema Mbowe

Aidha Mbowe aliendelea kusema kuwa 

"Maendeleo ya demokrasia yamerudi nyuma kwa kiasi kikubwa, tunakwenda kwenye uchaguzi huu, tumejiandaa kukabiliana na yeyote ambaye atatunyanyasa, kutuumiza ama kukiuka sheria katika kupendelea upande wowote kati ya pande zinazoshindania, ni rai yetu vyombo vyote vya  usalama na usimamizi vitekeleze majukumu yake kwa mujibu wa sheria tuko tayari kuheshimu.

Tutakapoona wenzetu ambao ni wasimamizi wa sheria, hawaheshimu washindani wenzao, wanaonea waziwazi wapinzani na wanabadilisha matakwa ya wananchi ili kupendelea chama fulani, watabadili mwelekeo wa uchaguzi huu. Wenzetu wakitaka tufanye siasa safi tutafanya, wakitaka kutumia vyombo vya dola kujipendelea na kutudhalilisha demokrasia nasi tutapambana kwa namna itakavyoruhusu"
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment