Mwalimu Akamatwa Kwa Kumpa Mimba Mwanafunzi

Mwalimu mmoja wa shule ya wanafunzi wenye ulemavu katika halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi, amefikishwa kwenye vyombo vya sheria kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mwanafunzi mwenye ulemavu na kumsababishia ujauzito.

Akizungumza katika kongamano la wadau wa elimu lililoandaliwa na shirika la TCRS, Mkuu wa wilaya Kilwa, Christopher Ngubiagai, amesema kitendo kilichofanywa na mwalimu huyo sio cha kukifumbia macho huku mwanafunzi akiwa amekatisha kuendelea na masomo yake.

Mkuu huyo wa wilaya pia, akaeleza wilaya yake inavyoathirika na tatizo la tatizo la mimba za utotoni na utoro na kupelekea kufanya vibaya katika mitihani ya Kimkoa na Kitaifa.

Wilaya hiyo imeshika nafasi ya sita kati ya wilaya sita za mkoa wa Lindi katika matokeo ya mithani wa darasa la Saba mwaka jana, huku ikishika nafasi ya 160 Kitaifa
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment