Ronaldinho Astaafu Soka Rasmi


Faridi Miraji.                                                     


Ronaldinho ameamua kustaafu soka rasmi akiwa na umri wa miaka 37 kauli iliyotolewa jana na kaka yake ambae pia ni wakala wake Roberto de Assis Moreira. 

Baada ya kukaa miaka miwili akiwa hana klabu ya kuichezea mwaka jana Ronaldinho alijitokeza na kusema mwaka 2018 ata achana na soka kama mchezaji na badala ya hapo atakuwa busy na mambo yake ya Music na kuangalia shule yake ya mpira. 

''Amestaafu kwasasa amemaliza kuishi kwenye maisha ya soka akiwa kama mchezaji" alisema Assis.

"Tutafanya kitu kizuri na kikubwa kwake baada ya michuano ya kombe la Dunia, nafikiri itakuwa mwezi August. Tutafanya   sherehe kubwa Brazil,  Europe na Asia na tumeandaa hicho kitu na timu ya Taifa ya Brazil tunahitaji ijumuike nasi"
Aliongeza Kaka yake

"Nike wadhamini wa muda mrefu wa Ronaldinho watakuwa pamoja na sisi kwenye project hii"
alisema kaka yake  Ronaldinho ambae pia ni wakala wake. 

Ronaldinho Ballon D'Or wa 2005 amechezea vilabu 8 na kufanikiwa kushinda makombe 13 katika maisha yake ya soka 
-Gremio 1998-2000
  Mechi 52 magoli 21
-PSG 2001-2003
  Mechi 55 magoli 17
-Barcelona 2003-2008
   Mechi 145 magoli 70
-Ac Milan 2008-2011
    Mechi 76 magolj 20
-Flamengo 2011-2012
  Mechi 33 magoli 15
-Atletico Mineiro 2012-2014
    Mechi 48 magoli 16
-Queretaro 2014-2015
    Mechi 28 magoli 5
-Fluminense 2015
    Mechi 7 magoli 0 

Timu ya taifa ya Brazil amecheza mechi 97 na kufunga magoli 33

(Jumla amecheza mechi  538 na kufunga magoli 200)

Ronaldinho ambaye alisema akistaafu soka  anajikita kwenye mziki kwa sasa
"Pindi nitakapo staafu nitaanza kuangalia zaidi Project zangu za music, na shule yangu ya mpira, ni vitu vipya kwangu, natakiwa kuvizoea."
Alisema Ronaldinho mwaka jana

Ronaldinho ameshinda makombe yafuatayo 
-UEFA intertoto Cup -2001 
-La liga 2004-2005
-La liga 2005-2006
-Supercopa De Espana 2005
-Supercopa de Espana 2006
-Uefa Chanpions League 2005-2006
-Seria A 2010-2011
-Copa Libertadores 2013
-Recopa Sudamericana 2014
-Copa America 1999
-Fifa world Cup 2002
-Fifa Confederation Cup 2005
-Fifa U17 World Championship 1997

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment