Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA, imekipiga faini kituo cha runinga cha Star TV ya jumla ya shilingi milioni 7.5 kwa makosa ya ukiukwaji wa taratibu za kutangaza taarifa ya habari, inayotakiwa kulipwa ndani ya siku 30 kuanzia leo.
Pia mamlaka hiyo imekiweka kituo hicho cha runinga kwenye uangalizi maalum kwa muda wa miezi sita kuanzia leo, kutokana na kurusha taarifa ya habari inayotajwa kuwa ya uchochezi.
Pia imekiadhibu kituo cha runinga cha Azam 2, kwa makosa ya kukiuka maadili ya uandishi wa habari na kurusha habari zenye uchochezi kuhusu uchaguzi wa madiwani
0 comments :
Post a Comment