Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) kimevishukia vyama vinavyounda Ukawa kufuatia uamuzi wake wa kushiriki uchaguzi mdogo wa Ubunge katika majimbo ya Kinondoni na Siha, baada ya kuususia uchaguzi huo kwa madai kuwa uchaguzi hautokuwa wa haki.
Akizungumza na wanahabari jana Januari 29, 2018 jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu wa TLP, Richard Lymo amedai kuwa, uamuzi huo wa UKAWA ambao umemsimamisha mgombea wa Chadema, Salum Mwalim kugombea jimbo la Kinondoni umewadanganya wananchi.
“Uamuzi huo umeonyesha kwamba Chadema haiheshimu wananchi, umedanganya wananchi na umeathiri upinzani. Walitangaza kujitoa halafu wamebadili gia angani kitendo hiki hakikubaliki,” alisema.
Lymo amedai kuwa, Chadema imesimamisha mgombea pasipo kufuata taratibu kutokana kwamba hakuna kikao kilichokaliwa wala maamuzi yaliyotolewa na vyama vinavyounda UKAWA katika kupendekeza mgombea wake.
“Katika uchaguzi huu hakuna UKAWA sababu iko vipande vipande, hakuna kikao au maamuzi ya UKAWA Chadema waliamua tu kutokana na maamuzi yao ya mwisho mwisho ya kushiriki uchaguzi. Kama wangesema hadharani sababu zilizowafanya kususia uchaguzi zimekwisha tusingepiga kelele,” alisema.
0 comments :
Post a Comment