Ukatili:Mtoto Aokotwa Akiwa Amefariki

Mtoto mchanga wa kiume anayesadikiwa kuwa na umri wa siku tatu ameokotwa akiwa amekufa baada ya kutupwa na watu wasiojulikan kwenye kichaka huko Tandale jijini Dar es salaam
Tukio hile limetokea siku ya mkesha wa mwaka mpya, ambapo Muuguzi wa Hospitali ya Mwananyamala Bi. Jasmine Malya amesema kuwa mtoto huyo ameokotwa na jeshi la polisi jijini Dar es salaam, na kuletwa katika hospitali hiyo akiwa tayari amefariki, na mwili wake kuhifadhiwa katika hospitali hiyo.
Licha ya tukio  hilo amesema kuwa jumla ya watoto saba wamezaliwa usiku wa kuamkia mkesha wa mwaka mpya wa 2018,  pamoja na kupokea majeruhi 11 wa ajali mbalimbali katika mkesha wa siku ya mwaka mpya.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment