Waandishi Wa Habari Waliotuhumiwa Kumtapeli Mganga Wa Kienyeji Wapewa Dhamana




Waandishi  wa habari wanne waliokamatwa kwa kujifanya maofisa usalama wa Taifa kutoka ikulu jijini Dar es saalam na kisha kujipatia shilingi milioni moja kutoka kwa mganga wa jadi leo wamepata dhamana katika mahakama ya Wilaya ya KahamaMbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya Wilaya Keneth Mtembei 

Alidai awali washitakiwa hao walipelekwa mahabusu baada ya kushindwa kukidhi vigezo vya dhamana ambavyo ni wadhamini wawili mmoja akiwa mtumishi wa serikali.. 

Hata hivyo Mtembei alisema mahakama ililegeza masharti hayo baada ya washitakiwa kuomba mahakama iwabadilishie masharti ya dhamana kutokana na kukosa wadhamini watumishi wa serikali. 

Kutokana na maombi hayo kwa kuzingatia washitakiwa wamekaa gerezani kwa mUda wa siku saba mahakama ilikubali maombi yao ya kubadilisha mashariti ya dhamana iKatoa nafasi kwa mdhamini yeyote mwenye mali isiyohamishika aweze kudhamini. Kufuatia hali hiyo hakimu Mtembei aliacha dhamana wazi kwa washitakiwa wote wanne kudhaminiwa na mtu yeyote mwenye mali isiyohamishika ndipo waandishi wa habari hao walipodhaminiwa kwa kila mmoja wadhamini wawili kwa shilingi milioni moja kila mmoja. 

Washitakiwa wote ambao ni Raymond Mihayo wa gazeti la Habari leo, Shaban Njia wa gazeti la Jambo leo na nipashe, Paul Kayanda wa gazeti la Uhuru, pamoja na Simon Dioniz wa Redio Kwizera wako nje kwa dhamana hiyo mpakaiJanuary 24 mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena katika mahakama hiyo. 

January 6 mwaka huu waandishi hawo wakiwa watano na mwenzao George Maziku aliyetoroka walifika nyumbani kwa mganga wa jadi Jane Mbeshi na kisha kumkamata kwamba anapiga ramli chonganishi na kisha kujipatia shilingi milioni moja na fedha nyingine kama hiyo ilibaki na Januari 9 walikwenda tena kwa lengo la kumalizia kupewa pesa hiyo ndipo walipokamatwa na polisi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment