Habari tulizozipokea hivi punde zinasema kuwa mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia leo alfajiri Ijumaa Februari 2,2018 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.
Mzee Kingunge alikuwa kiongozi mwandamizi nchini Tanzania katika serikali za awamu nne zilizopita naamewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika serikali zikiwemo ukuu wa mikoa ya Tanga na Singida, Katibu Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi na Waziri katika wizara mbalimbali.
Ndugu Kingunge Ngombale Mwiru atakumbukwa kwa kulitumikia taifa la Tanzania kwa uadilifu mkuu na uzalendo uliotukuka unaofaa kuigwa na vizazi vya sasa na vijavyo.
Taarifa zaidi tutawapatia hivi punde...
0 comments :
Post a Comment