Burundi Watumishi Waanza Kukatwa Mishahara Yao Kwaajili Ya Guarana Za Uchaguzi 2020

Wafanyakazi wa umma nchini Burundi wameanza kukatwa asilimia 10 ya mishahara yao kwaajili ya kufadhili uchaguzi mkuu unaotarajiwa mwaka 2020.
Katika kipindi cha miaka miwili ijayoraia wote wa Burundi walio na zaidi ya umri wa kupiga kura wa miaka kumi na minane na zaidini sharti wachangie katika hazina hiyo ya kitaifa.
Serikali ya Burundi imesema imechukua uamuzi huo ili kuziba pengo lililosababishwa na uamuzi wa wafadhili wa kuzuia misaada tangu mzozo wa mwaka 2015 wakati rais Pierre Nkurunziza alipowania muhula wa tatu.
Hata hivyo serikali imekariri kuwa hazina hiyo ya uchaguzi ni wazo la raia wa Burundi wenyewependekezo ambalo limepingwa na wakuu wa vyama vya wafanyakazi.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment