SIKU chache baada ya mrembo Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kutangaza kummwaga mpenzi wake, staa wa Bongo Fleva, Abdul Nasibu ‘Diamond Platnumz’, inasemekana kuwa, familia ya msanii huyo imewagomea wawili hao kuachana.
Taarifa ambazo Ijumaa lilizipata zilidai kuwa, ndugu wa Diamond hawakupendezwa na kitendo cha wawili hao kutengana kwa jinsi walivyokuwa wameshibana. “Familia imekataa kabisa.
Diamond na Zari hatua waliyokuwa wamefi kia si kwamba ni wachumba, bali ni mume na mke kwa sababu wamekaa pamoja kwa muda mrefu na ukizingatia tayari wana watoto wawili waliozaa pamoja,” Ijumaa lilitonywa.
Ijumaa lilielezwa kuwa, baadhi ya ndugu wa karibu wa Diamond wamekutana mara kadhaa na kulijadili suala hilo ili kuangalia uwezekano wa wawili hao kumaliza tofauti zao na kuishi kama zamani.
Gazeti hili lilielezwa kuwa, mbali na ndugu hao wa upande wa mama’ke Diamond, Sanura Kassim ‘Bi Sandra’, ndugu wengine wa upande wa baba yake Diamond, Abdul Jumaa nao Hawakufurahishwa na kitendo hicho.
“Ndugu wa baba Diamond nao hawakufurahia.
Baba Diamond mwenyewe licha ya kuwa ana mapenzi na mkwewe mwingine ambaye ni Hamisa Mobeto, lakini bado anataka mwanaye asimuache Zari,” Ijumaa lilielezwa katika uchunguzi wake.
Alipotafutwa baba Diamond, mzee Abdul Juma, alikiri kwamba kama familia hawakufurahishwa na jambo hilo na wanaangalia namna ya kuzungumza na mkwe wao (Zari) ili ikiwezekana wakae sawa.
“Nafanya bidiii ya kuwafi kia wenzangu kule (upande wa mama Diamond) ili ikiwezekana tuone namna ya kuwasuluhisha,” alisema baba Diamond.
Alipotafutwa mama Diamond kuhusu suala hilo, alipokea simu na kusikiliza kasha kupotea hewani na hata alipopigiwa tena, simu yake iliita bila kupokelewa.
Ijumaa pia lilimpigia simu kaka yake, Diamond, Romy Jons ili kumsikia anazungumziaje kuhusu suala hilo ambapo alipopatikana alisema: “Nipo hospitalini, naomba nikutafute baadaye.”
Hata hivyo, hadi muda unayoyoma, Romy hakurudi hewani hata alipotafutwa tena na Ijumaa, simu yake haikupatikan
Zari na Diamond (pichani) waliodumu kwenye uhusiano na kufanikiwa kuzaa watoto wawili, Tiffah na Nillan, walikuwa kwenye msuguano kwa kile kilichoelezwa kuwa ni usaliti aliokuwa akiufanya Diamond
Zari na Diamond (pichani) waliodumu kwenye uhusiano na kufanikiwa kuzaa watoto wawili, Tiffah na Nillan, walikuwa kwenye msuguano kwa kile kilichoelezwa kuwa ni usaliti aliokuwa akiufanya Diamond
Wakati anaandika waraka wa kummwaga Diamond, Zari alisema alifi kia uamuzi huo kutokana na Diamond kuwa na skendo nyingi za wanawake zinazoandikwa kwenye mitandao na vyombo vya habari.
0 comments :
Post a Comment