Na George Mganga
Baada ya mapumziko mafupi kupisha mashindano ya kimataifa, Ligi Kuu Soka Tanzania Bara itaendelea jioni ya leo kwa mchezo mmoja kupigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mechi ya leo, Simba ambayo ilisafiri Djibout kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikisho, leo itakuwa mwenyeji dhidi ya Mbao FC ya jijini Mwanza.
Kuelekea mchezo huo, Kocha wa Mbao, Etienne Ndayiragije, amesema kuwa leo ndiyo itakuwa siku ya kuvunja historia ya Simba kwa kuwachukulia pointi 3.
Ndayiragije ametamba kwamba leo ndiyo itakuwa mwisho wa Simba kuizua Mbao kupata alama 3 huku akieleza kuwa anaheshimu mchezo wa mpira kwamba una matokeo matatu.
Simba inaenda kucheza na Mbao ikiwa haijapoteza mchezo wowote wa Ligi mpaka sasa na ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 2-0 katika mechi ya raundi ya Mwanza iliyochezewa CCM Kirumba, Mwanza.
0 comments :
Post a Comment