Magufuli Amsaidia Mlemavu Bajaji

Rais waJamhuriya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kumsaidia Bajaj Mlemavu wa viungo Bw. Yusuf Abdulrahaman Ndemanga.
Bw. Ndemanga amekabidhiwa Bajaji hiyo na Katibu wa Rais Bw. Ngusa Samike, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 02 Februari, 2018.
Mhe. Rais Magufuli alikutanana Bw.Ndemanga tarehe 25 Agosti, 2017 katika sehemu ya abiria wakati akisubiri kupanda kivuko cha MV Magogoni kuelekea Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Mara baada ya kukutana na Mhe. Rais Magufuli, Bw. Ndemanga alimuomba msaada wakupatiwa Bajaj iliimsadie kupata kipato.
Akikabidhi msaada huo Bw. Ngusa Samike amemtaka Bw. Ndemanga kuitumia Bajaj hiyo vizuri nakujiongezea kipato kitakacho msaidia yeye na familia yake.
“Mhe. Rais amenituma nikukabidhi Bajaj hii mpya kabisa, matarajio yake nikuwa itakusaidia kupiga hatua za kimaendeleo, anatarajia kukuona unaongeza Bajaj nyingine na unaisaidia familia yako kupata nafuu ya maisha na sio kuja kuomba msaada mwingine”amesema Bw. NgusaSamike.
Kwa upande wake Bw. Ndemanga aliyeongozana na Mkewe Bi. Hawa Mohamed amemshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa msaada huo na ameahidi kuwa ataitumia Bajaj hiyo vizuri kuzalisha kipato kwa ajili ya familia yake.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment