TFF Yamfungia Kiongozi Wake

Shrikisho la soka Tanzania TFF kupitia kamati ya maadili leo imetangaza maamuzi yaliyowashitua wengi baada kutangaza kumuadhibu kwa kumfungia mwaka mmoja kutojihusisha na soka kiongozi wa timu ya Abajalo FC.
Kamati ya maadili ya TFF imetangaza kumfungia mwaka mmoja kujihusisha na soka na faini ya Tsh milioni tatu mwenyekiti wa club ya Abajalo FC Edgar Chibula kwa kosa la kuidhalilisha taasisi ya TFF.
Kikao cha January 28 2018 cha kamati ya maadili kilika na kujiridhisha kuwa Edgar Chibula anastahili kuadhibiwa kwa kosa alilofanya, taarifa ya kamati ya maadili inaeleza hivi.
“Shauri la Chibula ambaye ni mwenyekiti wa Abajalo limesikilizwa na kamati ambapo alishitakiwa kwa makosa ya kuikashifu, kuidhalilisha na kuivunjia heshima TFF kupitia vyombo vya habari ikiwa ni kinyume na taratibu na maadili ya TFF”
“Chimbula akiwa mwenyekiti wa Abajalo na mjumbe wa bodi ya ligi aliongea maneno ya kuikashifu, kuidhalilisha na kuivunjia heshima TFF katika vyombo vya habari akiwa kiongozi wa juu wa vyombo vya mpira hapa nchini na hakupaswa kuongea maneno ya kuikashifu taasisi anayoiongoza”
“Kwa kufanya hivyo anakuwa amevunja kanuni ya uwajibikaji wa pamoja na utunzaji siri za taasisi, katika shauri hilo mtuhumiwa hakuweza kuhudhuria na aliwasilisha utetezi kwa njia ya maandishi na kisheria unatambulika.”
“Secretariat iliwasilisha ushahidi wa sauti ambayo ilikuwa ni ya mahojiano na moja ya kituo cha redio ikiwa ni ushahidi ambapo katika mahojiano hayo mtuhumiwa alisikika akitamka maneno yasiyo na afya kwa mpira wetu”
Manara baada ya Yanga kupata penati “Baadhi ya maamuzi ni kichefuchefu”l
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment