Kutoka Houston, Texas, nchini Marekani, inaripotiwa kuwa askari mmoja amempiga risasi mwanaume mmoja asiye na silaha hadi kufariki ambaye alikuwa anatembea barabarani huku suruali yake ikiwa miguuni.
Kamera iliyonasa tukio hilo imemuonesha kijana huyo Danny Ray Thomas mwenye miaka 34, akitembea na polisi huyo kuanza kupiga kelele akimwambia lala chini na kisha akafyatua risasi na kumpiga.
Inaelezwa kuwa askari na mhanga huyo wa ‘ukatili wa polisi’ wote ni weusi wa Asili ya Afrika.
Familia ya marehemu, imeeleza kuwa ndugu yao alikuwa akitembea na suruali ikiwa miguuni kwasababu alikuwa anapitia msongo wa mawazo ‘depression‘ baada ya watoto wake kufariki
0 comments :
Post a Comment