Msanii wa muziki Bongo, Diamond amefunguka kuhusu kufungiwa kwa nyimbo zake mbili ‘Waka na Hallelujah’ kwa kueleza kuwa ni kitu ambacho hakiwezi kumpunguzia chochote na hakiwezi kujenga muziki wa Tanzania.
Muimbaji huyo ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa yupo tayari kupigania muziki wake kwa lolote lile na iwapo kuna sehemu ambayo wao kama wasanii wanaenda kinyume ni jambo la kuelekezana.
“Suala si kufungia tu nyimbo, mimi ukinifungia nyimbo hainipunguzii kitu nikienda nje naenda nai-perform ukiwa hutaki sinaondoka tu naenda nchi nyingine, kwa hiyo ni kukaa tuzungumze, tuelekezane lakini tusifanye kama kukomoana, hapana, tufanye katika mazingira ambayo yatasaidia sanaa ikue." Alisema Diamond na kuongeza;

"Huwezi kumfungia mtu kama roma kwa miezi sita,unajua kuwa anachangamoto gani?umeshawahi kutaka kuzitatua?
"Unanifungia nyimbo zangu umeshawahi kuchangia nini katika muziki wangu , utamnunulia tiffah wewe pampers?
"Simuogopi mtu hata kaka jela mimi nitaenda kwa ajili ya kuukomboa muziki .ntaitetea bongo fleva kwa sababu naijua kuliko anavyoijua yeye anaetufungia , sio unakuja unafungia bila hata kufanya research, anakuja na atatuacha sisi hapa."
Diamond ambae anaonekana kujiamini kuwa hata iweje lazima atasimama kwa ajili ya bongo fleva, anasema kuwa wala hajali kwa sababu hajapata taarifa rasmi juu ya kufungiwa kwa nyimbo zake zaidi ya kuziona habari katika mitandao ya kijamii
0 comments :
Post a Comment