Mkazi mmoja wa mkoani Iringa mwenye asili ya India, Hiren Shantilal Makvana mwenye umri wa miaka 29, amefariki dunia baada ya kujinyonga.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire, amesema tukio hilo limetokea Machi 26 mwaka huu katika makazi ya merehemu huyo ambaye alikuwa anaishi kwenye maghorofa ya NSSF Iringa, na kwamba marehemu alijinyonga kwa kutumia khanga, na mpaka sasa chanzo cha kufikia uamuzi huo bado hakijajulikna.
“Ni kweli siku ya Machi 26 tulipata taarifa za tukio hilo, na tulipoenda tulikuta marehemu ameshajinyonga, na alijinyonga kwa kutumia khanga, mke wake hakuwepo siku ya tukio ila taarifa zinasema kuwa amesafiri kwenda India, na hajaacha ujumbe wowote”, amesema Kamanda wa Polisi Juma Bwire.
Jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi kujua chanzo cha mtu huyo kuamua kujiua, na mpaka sasa jeshi la polisi halijapata taarifa zozote kutoka kwa ndugu zake wengine wa karibu.
0 comments :
Post a Comment