Wakati BASATA wakimtuhumu Diamond kulewa na umaarufu na kufanya abishae na Naibu waziri ambaye anawakilisha Serikali, bado huko katika mitandao ya kijamii watu wamezidi kuonyesha hisia zao juu ya jambo hilo kwa kudai kuwa Naibu waziri anatafuta kiki kwa lengo la Kumshusha Diamond.
Mwanahabari na Blogger, Le Mutuz ameibuka na kudai kwa Naibu Waziri amekuwa akitumiwa na watu wenye chuki kubwa na muziki wa Diamond ili kuua muziki wake na sio vinginevyo.
Le Mutuz anasema kuwa huu ulikuwa ni wakati wa serikali kuona mchango wa Diamond hasa baada ya kuchaguliwa kwenda kufanya show ya ufumbuzi wa kombe la Dunia.
Lemutuz ambaye amesema kuwa pamoja na kwamba Mh Juliana Shonza ni mwana CCM mwenzake lakini anaona kabis katika hili la kuwafungia na kubishana na Diamond katika mitandao ya kijamii hawezi kunyamaza kimya.
Hata hivyo Lemutuz amemhusisha Julana Shonza na moja ya kiongozi wa kituo fulani cha radio “MUNGU MTU” ambacho hajakitaja na kusema kuwa wamekuwa wakishirikiana ili kumtua Diamond katika nafasi kubwa ya mafanikio ya kimuziki aliyonayo.
0 comments :
Post a Comment