Msanii wa muziki wa injili nchini Emmanuel Mbasha amefunguka katika ukurasa wake wa instagram kwa kumuandikia barua ndefu aliyekuwa mke wake wa ndoa Florah Mbasha kuhusu kumnyima mtoto wake wa kike waliezaa nae walipokuwa wakikaa wote miaka ya nyuma.
Emanuel Mbasha na Flora Mbasha walifunga ndoa kanisani na kuishi pamoja na hata kufanya kazi zao za muziki wa injili pamoja lakini walikuja kuachana na hata kupelekana mahakamani kwa makosa ya kubaka ambapo baada ya upelelezi kukamilika ilikuja kuonekana kwamba Florah Mbasha alitunga kesi hiyo na kumsingizia mume wake hivvyo Emanuel Mbasha alichukua jukumu la kumtaliki mwanamke huyo.
Lakini Emanuel Mbasha anaonekana kuumia kukaaa mbali na mtoto wake wa kike walimpata na mzazi mwenzie huyo ambae alipewa mamlaka ya kukaa na mtoto huyo na mahakama kutokana na umri wa mtoto, Mbasha anasema kuwa pamoja na kwamba mahakama iliamuru mtoto kukaa na mama yake na yeye kuruhusiwa kumuona kwa muda tu lakini hata muda kidogo amekuwa akinyimwa na mzazi mwenzie huyo.
"Happy women’s day, ila ulinizalia mtoto mzuri mno nakushukuru sana,nimemmiss sana lizy unipage basi hata mtoto , unaninyima hata kumuona , karibia mwaka wa 2 unaelekea wa 3 sasa sijawahi kumuona mtoto daah mie babake tu ila naomba siku moja moja nifurahie maisha , aah nakuomba nimuone mwanangu lizy,najua hata mtoto amenimiss sana maana najua ameonoka kwangu akiwa mkubwa na nimemlea tamgu akiwa mtoto , atakuwa anshindwa tu kusema ila amenikumbuka sana.mahakama iliamua mtoto akae na mama ila niwe namuona mtoto ,sasa unapingana na mahakama…. sitaki povu hapa naongea na mzazi mwenzangu maana naona njia za kawaida zimeshinikana sasa inabidi nikuombe insta."
Mbasha anAsema kuwa ameamua kutuma ujumbe huo kwa Florah Mbasha ambae kwa sasa ameshaolewa na mwanaume mwingine kupitia instagram kwa sababu hakuna njia nyingine wanaweza kuwasiliana zaidi ya hiyo,
0 comments :
Post a Comment