Ujumbe wa Rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete katikati ya wiki hii uliteka mtandao wa kijamii wa Twitter na kusambaa kwenye Whatsapp, akionesha sehemu ya maisha yake baada ya urais.
Dkt. Kikwete ambaye alihamia Msoga mkoani Pwani kwa ajili ya mapumziko baada ya kutoka Ikulu, aliwepa picha kadhaa akiwa anakula chakula kwenye sahani na bakuli moja na wazee ambao walihudhuria msiba wa baba yake mdogo, Said Lumaliza katika kijiji cha Msigi.
“Tukila chakula na ndugu zangu msibani kwa baba yangu mdogo marehemu Said Lumaliza(1917-2018) katika kijiji cha Msigi karibu na Msoga. Hii ndiyo fahari ya maisha ya kustaafu.!” alitweet mara mbili kwa Kiswahili na Kiingereza, Machi 8.
Watumiaji wa mtandao huo ambao wengine walitoka nje ya nchi walisifu maisha ya kujishusha ya rais huyo mstaafu na kueleza kuwa ni viongozi wachache waliokuwa na cheo kama chake ambao wanaweza kurejea kwenye maisha ya aina hiyo.
“Kuna Maisha baada ya kustaafu. Itafika muda ulinzi kamili itakua ni yale uliyo wafanyia watu na ndicho nilicho jifunza hapo,” aliandika Samuel Isaya.
“Wewe ni rais wa mfano kwa Afrika pamoja na kuwa na mapungufu yako kama binadamu. Hongera sana mhe Mungu akutangulie ktk muda wote wa Maisha yako,” Zakayo Sarwatt.
0 comments :
Post a Comment