Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza amemfungia msanii Roma Mkatoliki kutojihusisha na tasnia ya muziki kwa kipindi cha miezi sita.
Akizungumza leo Machi 1, 2018 na baadhi ya wasanii aliowaita na kuwaeleza dosari zilizopo katika nyimbo zao, Shonza amesema baada ya Roma kupewa muda wa kufanya marekebisho wimbo wake wa Kibamia ameshindwa kutekeleza agizo hilo.
“Mpaka sasa hajaufanyia marekebisho na wimbo huo unaendelea kurushwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Tulitoa muda kwa Roma kufanyia marekebisho wimbo wake tangu mwaka jana mwishoni lakini mpaka leo ni miezi mitatu ameshindwa kutekeleza hilo,” amesema Shonza.
Amesema jana msanii huyo alipigiwa simu ili leo afike katika kikao hicho kwa ajili ya kujitetea, pia hakutokea.
0 comments :
Post a Comment